Psalms 12

Kuomba Msaada

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 a Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;
waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.
2 bKila mmoja humwambia jirani yake uongo;
midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

3 c Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila
na kila ulimi uliojaa majivuno,
4 dule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;
midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

5 e“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge
na kulia kwa uchungu kwa wahitaji,
nitainuka sasa,” asema Bwana.
“Nitawalinda kutokana na wale
wenye nia mbaya juu yao.”
6 fManeno ya Bwana ni safi,
kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,
iliyosafishwa mara saba.

7 gEe Bwana, utatuweka salama
na kutulinda na kizazi hiki milele.
8 hWatu waovu huenda wakiringa kila mahali
wakati ambapo yule aliye mbaya sana
ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.
Copyright information for SwhNEN